Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendige amewataka Wakutubi nchini kuwa kisima cha maarifa kipindi chote wanapokuwa wanatoa huduma ya kutoa taarifa kwa wasomaji.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Queen Sendige amewataka Wakutubi nchini kuwa kisima cha maarifa kipindi chote wanapokuwa wanatoa huduma ya kutoa taarifa kwa wasomaji.
Mhe. Sendige ameyasema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wakutubi Tanzani- Tanzania Library And Information Association (TLA)unaofanyika kwa siku 6 kuanzia 26 Februari - hadi 01 Machi 2024 katika ukumbu wa KISORA ROYOL HALL Wilayani Babati.
Katika hotuba yake ya Ufunguzi wa Mkutano huo akiwa kama mgeni rasmi Mhe. Sendige amewashukuru Viongozi wa Chama Cha Wakutubi Tanzani (TLA) kwa uamzi wao wa kuchagua Mkoa wa Manyara kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Wakutubi Tanzania kwa mwaka 2024.
Aidha Mhe. Sendige amewaasa Wakutubi kuwa kisima Cha maarifa mengi kwa kuwa wanahudumia wasomaji mbalimbali wenye uelewa tofauti, hivyo kuwaomba kuwa na maarifa mengi yatakayosaidia kujua vyanzo vingi vya taarifa ambazo wasomaji wanazihataji kupita kwao.
Aidha ametoa wito wa kuanzishwa Maktaba katika Mkoa wa Manyara Ili kuleta chachu ya usomaji katika jamii ya watu wa Manyara zikiwemo taasisi Serikali na Sekta binafsi.
"Naomba kuwashukuru sana kwa uwepo wenu kwa siku 6 katika Mkoa huu ni heshima ya pekee mmeupa Mkoa wetu heshima ya kufanya Mkutano wenu ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha usomaji kwa kuwa maarifa mengi yanapatikana kupitia kusoma vitabu na kupitia vyanzo mbalimbali kulingana na teknolojia tuliyonayo leo" ,Amesema Sendige.
Vile vile Mhe. Sendiga ametoa wito kwa viongozi wa TLA Mkutano ujao uwe na ushirikishwaji wa wadau wa sekta mbalimbali katika Ukutubi ili wasaidie kutoa maoni yao na kuanisha mapungufu yalipo kusoma vitabu wenyewe kwanza Ili waweze kuelewa maarifa yalimo
"Mtakuwa mmefanya jambo la maana sana kama mtawashirikisha wadau wenu wao ndio wanajua mafanikio na mapungufu yenu kuwashirikisha katika vikao vyenu watawasaidia sana kuinua tasania yenu hasa katika kipindi hiki ambacho teknolojia imepiga hautua kubwa" ,Amesema Sendiga
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi katika hotuba yake Makamu mwenyekiti wa TLA Dkt. Leontine kwa niaba ya Mwenyekiti wa TLA Prof Ally Mcharazo ameshukuru Mhe. Sendiga kwa kukubali mwaliko wa kuwa mgeni rasmi katika ufungunzi wa Mkutano huo.
Dkt. Leontine ameeleza kuwa Chama Cha Wakutubi Tanzani (TLA) kilianzishwa mnamo mwaka 1974 kikiwa na Malengo mengi kubwa ikiwa ni kuwakutanisha Wakutubi wote nchini ili waweze kijadili kwa pamoja mikakati na changamoto mbalimbali zinazoikabili Tasnia ya Ukutubi nchini.
Dkt. Nkebukwa ameeleza kuwa Chama Cha Wakutubi Tanzania (TLA) kimekuwa na mwendelezo wa kufanya mikutano yake kila mwaka kwa kuzunguka Kila Mkoa yote nchini isipokuwa Mkoa wa Manyara pekee ambao Mkutano huo unafanyika kwa mara ya kwanza.
MWISHO